Majaribio zaidi yanaendelea ya ndege mpya aina ya Boeing 787 Dreamliner yenye usajili 5H-TCR "The Great Serengeti Migration" kabla ya kukabidhiwa kwa mwendeshaji.
Pichani ni muendelezo wa majaribio hapo jana ambapo kwa mujibu wa FR24 inaonesha ilipangwa safari ya kutoka Charleston kuelekea Myrtle Beach, ingawa ilionekana kurudi kutua ilipoanzia safari.