Serikali ya Kenya imeruhusu Maduka ya Dawa za Binadamu kuanza kutoa huduma ya kwanza ya Dawa ya Kuzuia Maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI baada ua tafiti kuonesha zitasaidia Watu kuzipata kwa haraka na kuzitumia.
Majaribio yaliyofanywa chini ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI na Magonjwa ya Kuambukiza katika maeneo yenye maambukizi makubwa yamekuwa na matokeo chanya na Watumiaji wa dawa hizo kuongezeka.